Thursday 16 June 2016

Angalia Picha- Watoto na Vijana Kutoka Shinyanga na Simiyu Wakiendelea na Kambi ya Ariel Siku ya Pili Mkoani Kilimanjaro

1


Watoto na vijana 50 kutoka mikoa ya Shinyanga na Simiyu wameendelea na kambi yao mkoani Kilimanjaro ambapo katika siku ya pili Juni 14,2016 wamejifunza mada mbalimbali zinazolenga kuwapatia maarifa mbalimbali yatakayowawezesha kukua na kuishi katika matumaini chanya .

Kambi hiyo imeandaliwa na shirika la Ariel Glaser Pediatric Aids Healthcare Initiative (AGPAHI) linalojihusisha na mapambano dhidi ya Virusi vya Ukimwi (VVU) na Ukimwi katika mikoa ya Shinyanga,Simiyu na Geita.Pichani ni Afisa miradi huduma unganishi kwa jamii AGPAHI, Richard Kambarangwe akitoa mada kuhusu huduma na msaada wa kisaikolojia katika ukumbi wa Lutheran Uhuru Hotel mjini Moshi.Soma Habari Kamili Kuhusu Kambi ya Ariel <<HAPA>>
Watoto wakiimba wakati Afisa miradi huduma unganishi kwa jamii AGPAHI, Richard Kambarangwe akiendelea na mada yake
Afisa miradi huduma unganishi kwa jamii AGPAHI, Richard Kambarangwe akitoa mada ambapo alisema ushauri na msaada wa kisaikolojia unamsaidia watoto na vijana kubadilisha mtazamo na kujisikia huru katika maishaa na kuishi kwa furaha zaidi na kuwa na maisha bora zaidi
Watoto wakisikiliza kwa umakini kilichokuwa kinaendelea ukumbini
Afisa miradi huduma unganishi kwa jamii AGPAHI, Richard Kambarangwe akizungumzia mambo yanayoambata na msaada wa kisaikolojia kuwa ni pamoja na unyanyapaa na ukatili wa aina zote
Mshauri wa Masuala ya Kisaikolojia,Sherida Madanka akielezea masuala mbalimbali ya kisaikolojia
Meneja Mawasiliano na Huduma za Jamii kutoka AGPAHI, Jane Shuma akielezea maana ya mawasiliano wakati akitoa mada kuhusu mawasiliano kwa watoto na vijana
Kushoto ni mmoja wa vijana akieleza maana ya Mawasiliano mbele ya Meneja Mawasiliano na Huduma za Jamii kutoka AGPAHI, Jane Shuma(kushoto)

Meneja Mawasiliano na Huduma za Jamii kutoka AGPAHI, Jane Shuma (kushoto) akieleza maana ya mawasiliano
Meneja Mawasiliano na Huduma za Jamii kutoka AGPAHI, Jane Shuma akiwaelekeza vijana mchezo wa mawasiliano
Washiriki wa kambi hiyo wanaotoa msaada kwa watoto na vijana kambini wakiwa ukumbini
Watoto wakifuatilia kilichokuwa kinajiri ukumbini
Mkurugenzi wa miradi ya shirika la AGPAHI Tanzania, Dr. Amos Nsheha akitoa mada kuhusu taarifa sahihi juu ya Virusi vya Ukimwi na Ukimwi ambapo alisema endapo jamii itaelimishwa kuhusu VVU na Ukimwi itasaidia jamii kubadilika na kuamua kupima afya zao na baada ya hapo kama mtu atabainika kuwa ana maambukizi ya VVU basi ataanza kupata huduma ya tiba na matunzo na kama atakuwa hana maambukizi ya VVU basi atachukua tahadhali ili asipate maambukizi
Kijana akiuliza swali kuhusu VVU na Ukimwi kwa Mkurugenzi wa miradi ya shirika la AGPAHI Tanzania, Dr. Amos Nsheha
Tunafuatilia kinachoendelea .....
Mkurugenzi wa miradi ya shirika la AGPAHI Tanzania, Dr. Amos Nsheha akitoa elimu kwa vijana na watoto kuhusu VVU na Ukimwi
Wataalamu afya kutoka hospitali ya rufaa ya mkoa wa Shinyanga Dr.Anna Ndigawe(kushoto) na Mshauri wa Masuala ya Kisaikolojia,Sherida Madanka wakiwa ukumbini 
Kushoto ni Msimamizi wa vijana na watoto kutoka Kituo cha afya cha Muungano kilichopo wilaya ya Bariadi mkoani Simiyu Conjesta Mwijage akiwa maafisa miradi huduma unganishi kwa jamii AGPAHI, Richard Kambarangwe na Cecilia Yona wakiwa ukumbini
Washiriki wa kambi hiyo wakiwa ukumbini
Tunafuatilia kinachoendelea hapa.......
Mwandishi wa habari kutoka Radio Faraja ya Shinyanga Moshi Ndugulile akiwa ukumbini
Dr.Muta Mutakyawa kutoka AGPAHI akitoa mada kuhusu lishe
Watoto na vijana wakiwa wamesimama ukumbini
Msimamizi wa vijana na watoto kutoka Kituo cha afya cha Muungano kilichopo wilaya ya Bariadi mkoani Simiyu Conjesta Mwijage akiwa Afisa miradi huduma unganishi kwa jamii AGPAHI, Richard Kambarangwe 
Afisa miradi huduma unganishi kwa jamii kutoka AGPAHI, Cecilia Yona akitoa mada kuhusu haki za watoto-Picha zote na Kadama Malunde-Malunde1 blog

2